Kwa kuzingatia kifungu kikuu hapo juu, sasa nitajadili juu ya kuonekana kwa Mpinga Kristo na mauaji ya wafia-dini. Kuanzia sura ya 13 tunamwona Mnyama akitoka katika bahari. Huyu Mnyama, ambaye ana pembe kumi na vichwa 7 si mwingine bali ni Mpinga Kristo. Kifungu hiki kinatueleza kwamba juu ya pembe za yule Mnyama kulikuwa na vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake kulikuwa na majina ya makufuru. Pia tunaelezwa kwamba huyu Mnyama alikuwa ni kama chui, na miguu yake ikiwa kama miguu ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama mdomo wa simba. Kwa nyongeza, yule Joka akampatia nguvu zake, kiti chake cha enzi, na mamlaka makuu. Moja ya kichwa chake kilikuwa na jeraha la mauti, lakini hili jeraha la mauti lilipona kwa miujiza.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Ufunuo 8 inaeleza juu ya mapigo ambayo Mungu atayaleta juu ya dunia hii. Moja kati ya maswali ya msingi hapa ni kwamba watakatifu watahusishwa...
Neno la Ufunuo 11 ni la muhimu sana kwetu, ni muhimu kama lilivyo Neno lote la Mungu. Ili Mungu aweze kuuangamiza ulimwengu, basi kuna...
Katika sura ya 18 Mungu anatueleza kwamba atauangamiza mji ule mkubwa wa Babeli kwa mapigo yake makuu. Hii ni kwa sababu zitakapofikia nyakati za...