Mungu anatueleza kwamba wakati atakapoufanya ulimwengu huu kutoweka na kisha kutupatia Mbingu na Nchi Mpya, basi atamfufua kila mwenye dhambi aliyewahi kuishi hapa duniani na atakayekuwa amelala katika kaburi lake. Aya ya 13 inasema, “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.” Mwili wa mwanadamu unaozama katika maji mara huliwa na samaki, na mwili wa mwanadamu aliyeungua hadi kufa mwili wake mara nyingi utakuwa hauna umbile lolote la kuweza kutambuliwa na yeyote. Hata hivyo, Biblia inatueleza kwamba nyakati za mwisho zitakapowadia, Mungu atawafufua watu wote kurudi na kuwa hai na kisha atawahukumu ili kuwapeleka Mbinguni au kuzimu, hii haitajalisha ikiwa watakuwa wamemezwa na Shetani au la, au ikiwa watakuwa wameuawa na Jehanamu, au ikiwa watakuwa wameunguzwa na moto.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Sura ya 15 inatueleza juu ya mwisho wa ulimwengu utakaoletwa na mapigo ya mabakuli saba yatakayomiminwa na malaika saba. Je, hii “ishara nyingine katika...
Ufunuo 17:1-5 inasema, “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu...
Hii inatueleza juu ya Kanisa la Mungu likimpatia Mungu utukufu kwa kupitia kifo cha kuifia-dini. “Mwanamke aliyevikwa jua” ana maanisha ni Kanisa la Mungu...